Numbers 23:18-23

18 aNdipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki, inuka na usikilize,
nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori.

19 bMungu si mtu, hata aseme uongo,
wala yeye si mwanadamu, hata ajute.
Je, anasema, kisha asitende?
Je, anaahidi, asitimize?

20 Nimepokea agizo kubariki;
amebariki, nami siwezi kubadilisha.


21 “Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo,
wala taabu katika Israeli.
Bwana, Mungu wao yu pamoja nao,
nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.

22 Mungu aliwatoa kutoka Misri;
wao wana nguvu za nyati.

23 Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo,
wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli.
Sasa itasemwa kuhusu Yakobo
na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’
Copyright information for SwhKC